MAADHIMISHO YA
WIKI YA WAHANDISI TANZANIA – DODOMA.
(Motto: Uhandisi Kwa Maendeleo Ya Taifa)
![]() |
| Mh. Dr. Rehema Nchimbi Mkuu wa mkoa wa Dodoma akihutubia. |
Maadhimisho
yalifunguliwa na Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi. Katika
Hotuba yake Dr. Rehema Nchimbi alizungumzia umuhimu wa kazi za kihandisi
kutambulika na kuheshimika katika jamii yetu ya Tanzania na kwamba Maendeleo ya
Nchi yeyote Duniani huletwa na wahandisi. Aliwaomba watanzania wasibeze kazi
kubwa na nzuri zinazofanywa na wahandisi hapa nchini kwetu akitoa mifano ya
Majengo makubwa (magorofa) na Barabara nyingi na madaraja makubwa hapa Dodoma na Tanzania kwa ujumla ambazo zote zinajengwa
kwa kiwango cha Lami, alisema ni kazi kubwa inayofanywa na wahandisi.
Mheshimiwa aliwaomba
Wahandisi watumie taaluma yao walionayo ya uhandisi katika kurekebisha Maadili
ya Watoto na Vijana wa Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamemomonyoka .Aliendelea
kwa kusisitiza mtandao wa internet na utandawazi ambapo sasa karibia kila
mwananchi anaweza kuutumia umechangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa
maadili kwa vijana wetu.Alisema “kwa nini msitengeneze software (najua kuna
software Engineers) mvizuie hukohuko angani kabla havijawafikia watoto
wetu?...najua mkiamua mnaweza hebu fanyeni kitu hali ni mbaya”
Pamoja na maonyesho
hayo wahandisi wamejipanga kushiriki kikamilifu katika huduma mbalimbali za kijamii katika
wiki hii ikiwa ni pamoja na Kwenda katika shule za msingi na sekondari zilizoko
Dodoma mjini kufundisha masomo ya sayansi na kuwahamasisha wanafunzi wapende
masomo ya sayansi na fani ya Uhandisi kwa ujumla.Vile vile watashiriki katika
kufanya usafi wa mazingira maeneo ya Soko la Majengo Dodoma na kushiriki katika
katika Malumbano makubwa ya Hoja (Debate)
yatakayofanyika katika shule ya City High School siku ya Ijumaa saa 2.30
hadi saa 4,(Maada isemayo: Science Subjects are Better than Art Subject.)
![]() |
| Ufunguzi huo Uliambatana na Burudani mbalimbali ambapo kikundi cha ngoma Asilia cha “Hiari Ya Moyo” kilitumbuiza na kukonga nyoyo za watu walioohudhuria ufunguzi huo. |
![]() |
| Eng. Dr. M. Mzee na Eng. Musa Semwenda wakifuatilia kwa makini burudani kabambe ya ngoma asilia kutoka kwa kikundi cha “Hiyari Ya Moyo” Dodoma. |
![]() |
| Mh. Dr. Rehema Nchimbi akitembelea banda la TANROADS-Dodoma, Eng. Adelphina wa TANROADS akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya barabara mkoani Dodoma.Vile vile Mheshimiwa mkuu wa mkoa alitoa sifa kede kede kwa TANROADS jinsi walivyojipanga kuhakikisha barabara zote mjini hapa zinajengwa kwa kiwango cha Lami. |




Haya mhandisi....!
ReplyDelete