MAADHIMISHO YA
WIKI YA WAHANDISI TANZANIA – DODOMA.
(Motto: Uhandisi Kwa Maendeleo Ya Taifa)
 |
| Mh. Dr. Rehema
Nchimbi Mkuu wa mkoa wa Dodoma akihutubia. |
Maadhimisho
yalifunguliwa na Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi. Katika
Hotuba yake Dr. Rehema Nchimbi alizungumzia umuhimu wa kazi za kihandisi
kutambulika na kuheshimika katika jamii yetu ya Tanzania na kwamba Maendeleo ya
Nchi yeyote Duniani huletwa na wahandisi. Aliwaomba watanzania wasibeze kazi
kubwa na nzuri zinazofanywa na wahandisi hapa nchini kwetu akitoa mifano ya
Majengo makubwa (magorofa) na Barabara nyingi na madaraja makubwa hapa Dodoma na Tanzania kwa ujumla ambazo zote zinajengwa
kwa kiwango cha Lami, alisema ni kazi kubwa inayofanywa na wahandisi.
Mheshimiwa aliwaomba
Wahandisi watumie taaluma yao walionayo ya uhandisi katika kurekebisha Maadili
ya Watoto na Vijana wa Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamemomonyoka .Aliendelea
kwa kusisitiza mtandao wa internet na utandawazi ambapo sasa karibia kila
mwananchi anaweza kuutumia umechangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa
maadili kwa vijana wetu.Alisema “kwa nini msitengeneze software (najua kuna
software Engineers) mvizuie hukohuko angani kabla havijawafikia watoto
wetu?...najua mkiamua mnaweza hebu fanyeni kitu hali ni mbaya”
Hali Kadhalika Mheshimiwa
aliwasifia wahandisi kwa kuaandaa maadhimisho haya ambayo ndo yamefanyika kwa
mara ya kwanza mjini Dodoma na kuwa sio wachoyo kwa kuwaelimisha wananchi wa Dodoma pindi wanapotembelea
maonesho mbalimbali kwani kufanya hivyo
kunawaondolea wananchi hofu na kulaumu kusiko kwa lazima.Mfano alisema
“Wananchi wamekuwa na Fikra potofu kuwa
Wahandisi wanajenga madaraja usiku tu…wahandisi ni wachawi” au “Hii barabara
imejengwa ovyo yaani lami imewekwa chini halafu kokoto zinamwagwa juu……kumbe
kuna maelezo ya kitaalamu hapo yanoyoweza kuwaondolea wananchi wasiwasi”.
Aliwasihi wananchi wa Dodoma watembelee maonesho hayo yanayofanyika kwa wiki
nzima ili waulize maswali yao na watajibiwa na wataalamu katika mabanda mbali
mbali yaliopo viwanja vya Nyerere Square katikati kabisa ya mji wa Dodoma.
Pamoja na maonyesho
hayo wahandisi wamejipanga kushiriki kikamilifu katika huduma mbalimbali za kijamii katika
wiki hii ikiwa ni pamoja na Kwenda katika shule za msingi na sekondari zilizoko
Dodoma mjini kufundisha masomo ya sayansi na kuwahamasisha wanafunzi wapende
masomo ya sayansi na fani ya Uhandisi kwa ujumla.Vile vile watashiriki katika
kufanya usafi wa mazingira maeneo ya Soko la Majengo Dodoma na kushiriki katika
katika Malumbano makubwa ya Hoja (Debate)
yatakayofanyika katika shule ya City High School siku ya Ijumaa saa 2.30
hadi saa 4,(Maada isemayo: Science Subjects are Better than Art Subject.)
 |
| Ufunguzi huo
Uliambatana na Burudani mbalimbali ambapo kikundi cha ngoma Asilia cha “Hiari Ya Moyo” kilitumbuiza na
kukonga nyoyo za watu walioohudhuria ufunguzi huo. |
 |
| Eng. Dr. M. Mzee na
Eng. Musa Semwenda wakifuatilia kwa makini burudani kabambe ya ngoma asilia
kutoka kwa kikundi cha “Hiyari Ya Moyo” Dodoma. |
 |
| Mh. Dr. Rehema
Nchimbi akitembelea banda la TANROADS-Dodoma, Eng. Adelphina wa TANROADS akitoa
maelezo ya miradi mbalimbali ya barabara mkoani Dodoma.Vile vile Mheshimiwa
mkuu wa mkoa alitoa sifa kede kede kwa TANROADS jinsi walivyojipanga
kuhakikisha barabara zote mjini hapa zinajengwa kwa kiwango cha Lami. |