Monday, October 1, 2012

Analog to Digital Broadcasting Migration.


MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI KUTOKA ANALOJIA KWENDA DIJITALI

               

Utangulizi:      

- Kumbuka kuhama rasmi ni December 31, 2012. 

- Majaribio ya mfumo wa Dijitali yalianza kufanywa toka mwaka 2006 Mkoani Dodoma hivyo ni mpango uliokuwepo kwa muda mrefu.


Historia ya Utangazaji:

Utangazaji wa habari hapa Tanzania ulianza toka mwaka 1951, Kipindi hiki kulikuwa kuna kitu kinaitwa Voice of Dar es salaam-Mnazi mmoja pale. 
-        Kipindi hiki ilikuwa ukitakata kusikia habari ni lazima uende mnazi mmoja ambapo watu walikuwa wanakusanyika kupata habari ambapo matangazo ya habari  yalikuwa yanarushwa ‘Live’ kwa kutumia kipaza sauti
          -   Mwaka 1956 Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ilianzishwa baada ya uhuru 
          -  mwaka 1965 ikabadilishwa jina na kuitwa Radio Tanzania Dar es salaam(RTD) 
           -   Mwaka 1993 Sera ya Mawasiliano huru ilianzishwa hapa vikaibuka vyombo mbalimbali vya habari TV na Radio za watu Binafsi.

Kutoka Mwaka 1993 mpaka sasa Tanzania tuna vituo vya kurusha matangazo ya radio visivyozidi 80 na Television zisizozidi 30.

Teknolojia ya Analojia

Kwa ufupi hatuwezi kuiepuka teknolojia ya Analojia moja kwa moja kwani Macho yetu yana uwezo wa kuona picha zilizo kwenye mfumo wa Analojia Halikadhalika Masikio yetu yanasikia sauti iliyo katika mfumo wa analojia. Hivyo kinachobadilika ‘exactly’ ni namna haya matangazo yatakavyokuwa yanasafirishwa (Masafa) kutoka kituo cha matangazo hadi kumfikia mtazamaji.

Mapungufu Ya Analojia/Faida za Dijitali(Andavantages of Digital Broadcasting)

 

     1)      Matumizi Mabaya ya Masafa (‘Bandwidth’) 
-Hii ni rasilimali ambayo kila mtu anaitaka ili aweze kurusha matangazo, Tanzania sasa kila mtu/Taasisi na jumuiya mbalimbali wanataka kuanzisha TV zao na matokeo yake haya masafa yanakuwa hayatoshi.Kwenye Dijitali masafa moja inatumika kusafirisha Channel (TV) nyingi.(Channel Encoding and Decoding).
 
     2)      Uingiliano wa Masafa (Confidentiality)
-Usiri unaongezeka kwenye Dijitali kwani hakuna kuingiliana na utahitaji Decoder husika uweze kupata matangazo husika. 

 3)   Matumizi makubwa ya Umeme (High power consuption) 
           Umeme wa kusafirisha Chanel moja unaweza kutumika kusafirisha channel hadi 20 Kwenye mfumo wa Dijitali.
    4)      Ubora wa sauti na picha kwenye mfumo wa Dijitali kuliko Analojia.
    5)      Parental Control.
Unauwezo wa kuchagua channel zipi ziangaliwe na watu gani kwa wakati gani mfano; watoto, channel za dini, Michezo  n.k.   ukiwa katika mfumo wa Dijitali. 
    6)      Huduma nyingi za ziada- Tunapozungumzia dijitali tunazungumzia IP Television hapa tutaweza kutumia mtandao wa internet kupitia TV zetu (sina haja ya kutaja faida za mtandao wa internet kwani wote mnazijua).

Picture showing  Digital TV being used in Managing Bank account, Shopping Online etc.
  
    Upokeaji wa Matangazo ya Dijitali (Receiving Digital Broadcasting)

Ili uweze kupata matangazo ya Dijitali kwenye TV yako inatakiwa uwe na King’amuzi (Decoder) au uwe na Digital Ready TV.


  •         King’amuzi (Decoder)
Mpaka sasa Serikali kupitia TCRA imeshatoa Leseni 3  kwa wadau (Shareholders) wa mfumo huu mpya wa Dijitali TV.ambao ni ;
                 1)  Star Times (TBC) – Hawa tayari wameshaanza kufanya kazi na ving’amuzi vyao
                               Vipo madukani.

2) Ting (ATN)  - Hawa pia wapo tayari  na Ving’amuzi vyao vipo madukani.

3)   Basic Media (jointly ITV & Star TV)

 Hawa wanamalizia kuweka miundo mbinu mda si mrefu Ving’amuzi vyao vitakuwaMadukani.

N.B:
Kila leseni moja inampa mdau mmoja uwezo wa kurusha TV 300, Hivyo tutakuwa na uwezo wa kuwa na Television 900……huh.!
   
  •        Digital Ready TV
Hizi ni Luninga ambazo ving’amuzi vipo tayari ndani yake (Built in)…hapa ndugu zangu tuwe makini kwani mataperi wataibuka na kuuzia watu TV za kawaida kwa bei ya digital ready TV.
Digital Ready TV huwa zimeandikwa (labelled);
ü  DVB- T Tuner
ü  DVB-T2 Tuner

     Mafanikio

             Mafanikio ni makubwa sana kwani kampuni tatu zishapewa leseni, 2 tayari zinafanya kazi na moja ndo wanamalizia miundo mbinu.
-   Ifahamike kwamba katika mfumo tulionao wa Analojia ni asilimia 28 (28%) tu ya Watanzania wote walikuwa na uwezo wa kupata matangazo ya Television. 
-   Digital Television Coverage yake mpaka sasa ni 24% ya watanzania wote na ikikamilika coverage itakuwa ni 98% . 


Changamoto


-  Ulimwengu Mzima una-change kwenda kwenye mfumo wa Dijitali kutoka Analojia kwa hiyo Tukichelewa tuu sisi ndo tutakuwa Dampo la vifaa vya electronics vya Analojia (CRT) (since they can’t be recycled).

 -  Ving’amuzi vinashuka bei – kadri uhitaji (demand) unavyokuwa mkubwa siku zote bei huwa inashuka hivyo jipatie king’amuzi chako sasa.

 -  Content za TV ili tuweze kujaza hizo channel 900 hii nichangamoto kubwa sana kwani kutoka channel 30 za sasa kwenda hadi 900…huh..!

Opportunity


    Watanzania Tubadilike na tuanze kuandaa Contents za TV na kuwauzia hao mashareholder watatu waweze kuzijaza channel 900. Ili hizi TV zetu ziwe na contents nyingi ziwe zinazoendana na maadili ya kitanzania kuliko kuachia TV za nje tuu ndo zijaze hizi channel 900.
 

Mwisho Kabisa
  
   -   Serikali iendelee na huu mpango wa kuhama 
  -    Watu tukubaliane na tuhame.











    "Is the Post Helpful.....Tell a Friend!.....And if You still have any Doubt/Questions/A Word,  just leave me  comments"

Thursday, September 27, 2012

TEACHING PUPILS..!


HELPING PUPILS IN  MATHEMATICS AND SCIENCE SUBJECTS AT MAKOLE PRIMARY SCHOOL.


These are Standard Six pupils from Makole Primary School, the Task for today is to make them love Mathematics  as well as Science Subjects so that they will become future Engineers....!hhuh!


Ok....!Let's keep going and that is our Topic for Today (Geometry)...Kofia Huuzwa Dukani Mwa Daudi Senti Mia moja..."We sing together the song"



Are We Clear.?I asked them after several Demostratio...."Yees" but i see Sad faces I spoke to myselfi have to do something here..!Huh...!


Keep on Remonstrating Giving them more and more tricks to solve the problems....!


I start to see smiling faces...yeah..!Nimeeleweka...!

Busy Doing Exercise........!

Waoooh..!!Everybody is Happy now after finding the secrets behind mathematics....!All were very inspired and promised that they will never worry about mathematics and Science subjects again...!


Waving a goodbye to them.....!"Teacher are going to come back again tommorow..?"they asked..and I said "No thank you i have other responsibility at my duty station" but i promised them once i get a chance in the future i will be happy to comeback and teach them again oneday..!huh.!





Wednesday, September 26, 2012

IET Week - Dodoma 2012



MAADHIMISHO YA WIKI YA WAHANDISI TANZANIA – DODOMA.
       (Motto: Uhandisi Kwa Maendeleo Ya Taifa)

Mh. Dr. Rehema Nchimbi Mkuu wa mkoa wa Dodoma akihutubia.
Maadhimisho yalifunguliwa na Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi. Katika Hotuba yake Dr. Rehema Nchimbi alizungumzia umuhimu wa kazi za kihandisi kutambulika na kuheshimika katika jamii yetu ya Tanzania na kwamba Maendeleo ya Nchi yeyote Duniani huletwa na wahandisi. Aliwaomba watanzania wasibeze kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na wahandisi hapa nchini kwetu akitoa mifano ya Majengo makubwa (magorofa) na Barabara nyingi na madaraja makubwa hapa Dodoma  na Tanzania kwa ujumla ambazo zote zinajengwa kwa kiwango cha Lami, alisema ni kazi kubwa  inayofanywa na wahandisi.

Mheshimiwa aliwaomba Wahandisi watumie taaluma yao walionayo ya uhandisi katika kurekebisha Maadili ya Watoto na Vijana wa Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamemomonyoka .Aliendelea kwa kusisitiza mtandao wa internet na utandawazi ambapo sasa karibia kila mwananchi anaweza kuutumia umechangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa maadili kwa vijana wetu.Alisema “kwa nini msitengeneze software (najua kuna software Engineers) mvizuie hukohuko angani kabla havijawafikia watoto wetu?...najua mkiamua mnaweza hebu fanyeni kitu hali ni mbaya”

Hali Kadhalika Mheshimiwa aliwasifia wahandisi kwa kuaandaa maadhimisho haya ambayo ndo yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma na kuwa sio wachoyo kwa kuwaelimisha  wananchi wa Dodoma pindi wanapotembelea maonesho mbalimbali  kwani kufanya hivyo kunawaondolea wananchi hofu na kulaumu kusiko kwa lazima.Mfano alisema “Wananchi wamekuwa na Fikra potofu kuwa  Wahandisi wanajenga madaraja usiku tu…wahandisi ni wachawi” au “Hii barabara imejengwa ovyo yaani lami imewekwa chini halafu kokoto zinamwagwa juu……kumbe kuna maelezo ya kitaalamu hapo yanoyoweza kuwaondolea wananchi wasiwasi”. Aliwasihi wananchi wa Dodoma watembelee maonesho hayo yanayofanyika kwa wiki nzima ili waulize maswali yao na watajibiwa na wataalamu katika mabanda mbali mbali yaliopo viwanja vya Nyerere Square katikati kabisa ya mji wa Dodoma.


Pamoja na maonyesho hayo wahandisi wamejipanga kushiriki kikamilifu katika huduma mbalimbali za kijamii katika wiki hii ikiwa ni pamoja na Kwenda katika shule za msingi na sekondari zilizoko Dodoma mjini kufundisha masomo ya sayansi na kuwahamasisha wanafunzi wapende masomo ya sayansi na fani ya Uhandisi kwa ujumla.Vile vile watashiriki katika kufanya usafi wa mazingira maeneo ya Soko la Majengo Dodoma na kushiriki katika katika Malumbano makubwa ya Hoja (Debate)  yatakayofanyika katika shule ya City High School siku ya Ijumaa saa 2.30 hadi saa 4,(Maada isemayo: Science Subjects are Better than Art Subject.)

Ufunguzi huo Uliambatana na Burudani mbalimbali ambapo kikundi cha ngoma Asilia cha  “Hiari Ya Moyo” kilitumbuiza na kukonga nyoyo za watu walioohudhuria ufunguzi huo.

Eng. Dr. M. Mzee na Eng. Musa Semwenda wakifuatilia kwa makini burudani kabambe ya ngoma asilia kutoka kwa kikundi cha “Hiyari Ya Moyo” Dodoma.



Mh. Dr. Rehema Nchimbi akitembelea banda la TANROADS-Dodoma, Eng. Adelphina wa TANROADS akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya barabara mkoani Dodoma.Vile vile Mheshimiwa mkuu wa mkoa alitoa sifa kede kede kwa TANROADS jinsi walivyojipanga kuhakikisha barabara zote mjini hapa zinajengwa kwa kiwango cha Lami.