Monday, October 1, 2012

Analog to Digital Broadcasting Migration.


MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI KUTOKA ANALOJIA KWENDA DIJITALI

               

Utangulizi:      

- Kumbuka kuhama rasmi ni December 31, 2012. 

- Majaribio ya mfumo wa Dijitali yalianza kufanywa toka mwaka 2006 Mkoani Dodoma hivyo ni mpango uliokuwepo kwa muda mrefu.


Historia ya Utangazaji:

Utangazaji wa habari hapa Tanzania ulianza toka mwaka 1951, Kipindi hiki kulikuwa kuna kitu kinaitwa Voice of Dar es salaam-Mnazi mmoja pale. 
-        Kipindi hiki ilikuwa ukitakata kusikia habari ni lazima uende mnazi mmoja ambapo watu walikuwa wanakusanyika kupata habari ambapo matangazo ya habari  yalikuwa yanarushwa ‘Live’ kwa kutumia kipaza sauti
          -   Mwaka 1956 Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ilianzishwa baada ya uhuru 
          -  mwaka 1965 ikabadilishwa jina na kuitwa Radio Tanzania Dar es salaam(RTD) 
           -   Mwaka 1993 Sera ya Mawasiliano huru ilianzishwa hapa vikaibuka vyombo mbalimbali vya habari TV na Radio za watu Binafsi.

Kutoka Mwaka 1993 mpaka sasa Tanzania tuna vituo vya kurusha matangazo ya radio visivyozidi 80 na Television zisizozidi 30.

Teknolojia ya Analojia

Kwa ufupi hatuwezi kuiepuka teknolojia ya Analojia moja kwa moja kwani Macho yetu yana uwezo wa kuona picha zilizo kwenye mfumo wa Analojia Halikadhalika Masikio yetu yanasikia sauti iliyo katika mfumo wa analojia. Hivyo kinachobadilika ‘exactly’ ni namna haya matangazo yatakavyokuwa yanasafirishwa (Masafa) kutoka kituo cha matangazo hadi kumfikia mtazamaji.

Mapungufu Ya Analojia/Faida za Dijitali(Andavantages of Digital Broadcasting)

 

     1)      Matumizi Mabaya ya Masafa (‘Bandwidth’) 
-Hii ni rasilimali ambayo kila mtu anaitaka ili aweze kurusha matangazo, Tanzania sasa kila mtu/Taasisi na jumuiya mbalimbali wanataka kuanzisha TV zao na matokeo yake haya masafa yanakuwa hayatoshi.Kwenye Dijitali masafa moja inatumika kusafirisha Channel (TV) nyingi.(Channel Encoding and Decoding).
 
     2)      Uingiliano wa Masafa (Confidentiality)
-Usiri unaongezeka kwenye Dijitali kwani hakuna kuingiliana na utahitaji Decoder husika uweze kupata matangazo husika. 

 3)   Matumizi makubwa ya Umeme (High power consuption) 
           Umeme wa kusafirisha Chanel moja unaweza kutumika kusafirisha channel hadi 20 Kwenye mfumo wa Dijitali.
    4)      Ubora wa sauti na picha kwenye mfumo wa Dijitali kuliko Analojia.
    5)      Parental Control.
Unauwezo wa kuchagua channel zipi ziangaliwe na watu gani kwa wakati gani mfano; watoto, channel za dini, Michezo  n.k.   ukiwa katika mfumo wa Dijitali. 
    6)      Huduma nyingi za ziada- Tunapozungumzia dijitali tunazungumzia IP Television hapa tutaweza kutumia mtandao wa internet kupitia TV zetu (sina haja ya kutaja faida za mtandao wa internet kwani wote mnazijua).

Picture showing  Digital TV being used in Managing Bank account, Shopping Online etc.
  
    Upokeaji wa Matangazo ya Dijitali (Receiving Digital Broadcasting)

Ili uweze kupata matangazo ya Dijitali kwenye TV yako inatakiwa uwe na King’amuzi (Decoder) au uwe na Digital Ready TV.


  •         King’amuzi (Decoder)
Mpaka sasa Serikali kupitia TCRA imeshatoa Leseni 3  kwa wadau (Shareholders) wa mfumo huu mpya wa Dijitali TV.ambao ni ;
                 1)  Star Times (TBC) – Hawa tayari wameshaanza kufanya kazi na ving’amuzi vyao
                               Vipo madukani.

2) Ting (ATN)  - Hawa pia wapo tayari  na Ving’amuzi vyao vipo madukani.

3)   Basic Media (jointly ITV & Star TV)

 Hawa wanamalizia kuweka miundo mbinu mda si mrefu Ving’amuzi vyao vitakuwaMadukani.

N.B:
Kila leseni moja inampa mdau mmoja uwezo wa kurusha TV 300, Hivyo tutakuwa na uwezo wa kuwa na Television 900……huh.!
   
  •        Digital Ready TV
Hizi ni Luninga ambazo ving’amuzi vipo tayari ndani yake (Built in)…hapa ndugu zangu tuwe makini kwani mataperi wataibuka na kuuzia watu TV za kawaida kwa bei ya digital ready TV.
Digital Ready TV huwa zimeandikwa (labelled);
ü  DVB- T Tuner
ü  DVB-T2 Tuner

     Mafanikio

             Mafanikio ni makubwa sana kwani kampuni tatu zishapewa leseni, 2 tayari zinafanya kazi na moja ndo wanamalizia miundo mbinu.
-   Ifahamike kwamba katika mfumo tulionao wa Analojia ni asilimia 28 (28%) tu ya Watanzania wote walikuwa na uwezo wa kupata matangazo ya Television. 
-   Digital Television Coverage yake mpaka sasa ni 24% ya watanzania wote na ikikamilika coverage itakuwa ni 98% . 


Changamoto


-  Ulimwengu Mzima una-change kwenda kwenye mfumo wa Dijitali kutoka Analojia kwa hiyo Tukichelewa tuu sisi ndo tutakuwa Dampo la vifaa vya electronics vya Analojia (CRT) (since they can’t be recycled).

 -  Ving’amuzi vinashuka bei – kadri uhitaji (demand) unavyokuwa mkubwa siku zote bei huwa inashuka hivyo jipatie king’amuzi chako sasa.

 -  Content za TV ili tuweze kujaza hizo channel 900 hii nichangamoto kubwa sana kwani kutoka channel 30 za sasa kwenda hadi 900…huh..!

Opportunity


    Watanzania Tubadilike na tuanze kuandaa Contents za TV na kuwauzia hao mashareholder watatu waweze kuzijaza channel 900. Ili hizi TV zetu ziwe na contents nyingi ziwe zinazoendana na maadili ya kitanzania kuliko kuachia TV za nje tuu ndo zijaze hizi channel 900.
 

Mwisho Kabisa
  
   -   Serikali iendelee na huu mpango wa kuhama 
  -    Watu tukubaliane na tuhame.











    "Is the Post Helpful.....Tell a Friend!.....And if You still have any Doubt/Questions/A Word,  just leave me  comments"

2 comments:

  1. thanks broo kwa post nzuri but katika changamoto hapo ya tatu hapo hebu isome vzuri utagundua kitu,..
    na ninaomba if possible uje na part 2 ya hii post uzungumzie matangazo ya sattelite ( hz free to air) na hatma yake na kuhusu utaratibu wa jamaa kununua tv contents, nn kinahtajika kwa mtu kuwa na tv station, na utaratibu mzima wa malipo ya matangazo ukihusisha mwananch,hawa wenye vng'amuzi na mwenye tv sation(contents)

    ReplyDelete
  2. OK, nimekupata Baraka Emmanuel....Kwa ufupi matangazo ya sattelite huwa tayari yapo kwenye digital na ndio maana huwa unahiji Decoder husika uweze kuyapata, hata watu wanaotumia Cable TV nao hawatahusika na zoezi hili kwani tayari walishaingia kwenye Digital.Na TV station ambazo ni free to air(ITV,star TV.channel Ten N.K) zitapatikana kwenye Ving'amuzi vyote na kama hutalipa monthly fee ya king'amuzi utaendelea kuzipata.
    TV contents- unaweza kubuni programu yeyoyote(vichekesho, tamthilia, elimu)angalia mfano kama Isidingo wenyewe wanaandaa contents wanawauzia ITV kwa hyo contents zikiwa nyingi chanel nyingi na nyingi zaidi zitatumika.

    ReplyDelete